Wema Sepetu Adaiwa Million 70

Jumba la kifahari linalodaiwa kumilikiwa na mwanadada ambaye fedha imemtembelea, Wema Isaac Sepetu limesababisha staa huyo kuwa na deni la Sh. milioni 70.
Akizungumza na gazeti hili katika spesho intavyu, Wema ambaye siku hizi wanamwita Jaji Sepetu kutokana na kuwa jaji katika mashindano mengi ya ‘umisi’ yaliyofanyika hivi karibuni alisema kuwa yeye ndiye mtu wa mwisho katika kusema ukweli juu ya nyumba yake hiyo iliyopo Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama ‘Hollywood’ jijini Dar.

TUJIUNGE NA WEMA
Akibumburua siri nzito juu ya jumba hilo, Jaji Sepetu alisema: “Kusema kweli nilipopelekwa kwenye ile nyumba kwa mara ya kwanza sikuwa na wazo la kuinunua. Nilitaka kupangisha tu lakini wazo hilo lilikuja baada ya kuhamia na kushawishiwa na injinia aliyekuwa akinidizainia.”

IMENUNULIWA MIL. 280
“Watu wanasema naongopa kuwa nimenunua nyumba Sh. milioni 400, sina sababu ya kudanganya kwani ukweli ni kwamba nyumba niliinunua Sh. milioni 280.
“Sh. milioni 400 ilifika baada ya kuidizaini na kuingiza samani mpya.

AHAHA KULIPA
DENI MIL. 70
“Hata hivyo, sikumaliza kulipa fedha zote, tulikubaliana nilipe kwa awamu, hapa nilipo nahaha kulipa deni lililobaki la Sh. milioni 70.
“Kwa wale wanaohitaji kuona hati wasubiri nikimalizia deni nitakabidhiwa hati ya nyumba na nawahakikishieni nitakuwa nimewafunga mdomo wanaoeneza habari zisizo na kichwa wala miguu.”

WEMA UNAPATA
WAPI FEDHA?
Hebu msikie staa huyo aliyemdondosha Bongo mwigizaji mkubwa wa Nollywood, Nigeria, Omotola Jalade hivi karibuni:
“Kuhusu ninakopata fedha, hiyo ni siri yangu na katika maisha yangu hujawahi kusikia nahusishwa na mambo Freemason ila ifahamike nafanya sana kazi kutafuta shilingi.”

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

`
Design By : Tanzania Servers Technology