Waislamu Ufaransa walaani ubaguzi Ramadhani

Posted on Aug 5 2012 - 10:13am by Mwemutsi Erick

Kumefanyika maandamano makubwa nchini Ufaransa kupinga kitendo cha kufutwa kazi Waislamu wanne kwa sababu ya kufunga saumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Waislamu hao walikuwa wakitoa mafunzo katika kambi ya watoto mjini Geenevilliers nje kidogo ya mji mkuu wa Ufaransa, Paris. Waislamu wameandamana nje ya baraza la mji huo wakilaani kiteno cha kufutwa kazi Waislamu hao. Maafisa wa elimu mjini humo walidai kuwa kutokula na kunywa kunawazuia waalimu kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Baraza Kuu la Waislamu Ufaransa limekosoa vikali hatua ya kuwafuta kazi Waislamu hao na kusema saumu ni haki ya kimsingi ya Waislamu. Msemaji wa CFCM Abdallah Zekri amesisitiza kuwa uhuru wa kuabudu ni haki ya kimsingi na kwa vyovyote vile hakuna haki ya kumpiga mtu marufuku kutekeleza maamrisho ya dini yake. Waislamu Ufaransa wamekuwa wakilalamika kuwa wanabaguliwa sana. Mwaka 2004 Ufaransa ilipiga marufuku uvaaji wa Hijabu katika maeneo ya umma na nchi kadhaa za Ulaya pia zikaiga mfano huo mbaya.  Aidha Waislamu wa maeneo kadhaa ya Ufaransa wamenyimwa ruhusa ya kujenga misikiti au kuswali nje wakati misikiti inapojaa.

Leave A Response