Waasi Nigeria wateka raia wanne wa kigeni

Waasi nchini Nigeria wamewateka nyara raia wanne wa kigeni na kuua maafisa wawili wa jeshi la wanamaji nchini humo katika shambulizi dhidi ya meli ya Shirika la Mafuta la Sea Truck la Uholanzi. Msemaji wa Jeshi la Wanamaji la Nigeria Kabir Aliyu amethibitisha kutokea hujuma hiyo lakini hakutaja uraia wa waliotekwa nyara. Waasi katika eneo la Niger Delta lenye utajiri mkubwa wa mafuta wamekuwa wakiwateka nyara raia wa kigeni. Wakaazi wa Niger Delta wanalalamika kuwa pamoja na kuwa katika eneo lenye utajiri wa mafuta bado wanaishi katika umasikini wa kupindukia. Nigeria ni mwanachama wa Shirika la Nchi Zinazouza Mafuta kwa Wingi Duniani OPEC na inakadiriwa nchi hiyo huzalisha karibu mapipa milioni 2.4 ya mafuta kwa siku. Ufisadi mkubwa nchini Nigeria husababisha ubadhirifu wa pato la mafuta.

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

`
Design By : Tanzania Servers Technology