Ugiriki yapiga kura, euro mashakani

Posted on Jun 18 2012 - 12:10am by Mwemutsi Erick

Wakati Wagiriki wakipiga kura leo (17.06.2012) katika uchaguzi unaoweza kuamua hatima ya taifa hilo katika sarafu ya euro, kushindwa kwa vyama vya kisiasa kutafuta msimamo wa pamoja kunaonyesha hali ya mtafaruku.

Wagombea wakuu, chama cha kihifidhina cha New Democracy na Syriza chama cha nadharia za mrengo wa kushoto, vimeahidi kila kimoja kuunda serikali ambayo itajadili upya masharti magumu ya mkopo wa kuiokoa nchi hiyo uliotolewa na umoja wa Ulaya na shirika la fedha la kimataifa IMF, lakini wanataka kufanya hivyo kwa masharti yao binafsi.