Ni Yanga na Azam FC,Kagame fainali

Mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame Yanga wamefanikiwa kuingia hatua ya fainali katika mashindano ya soka yanayoendelea jijini Dar es salaam nchini Tanzania.


Yanga ya Dar es Salaam imefanikiwa kufika fainali baada ya kuifunga kwa taabu timu ya APR ya Rwanda bao 1-0 katika uwanja wa Taifa jijini humo.Baada ya ushindi huo Yanga sasa Jumamosi itakabiliana na timu ya Azam FC nayo ya Dar es Salaam ambayo ilipata nafasi hiyo ya kuingia fainali baada ya kuibamiza Vita FC ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bao 2-1.

Timu ya Vita na APR zitacheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu siku hiyo kabla ya mchezo wa fainali baada ya kupoteza mechi zao za leo.

Yanga kama itashinda mchezo wake huo wa fainali itakuwa imetwaa ubingwa huo mara mbili mfululizo kwani ndio mabingwa watetezi.

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

`
Design By : Tanzania Servers Technology