Ndege za kivita za Marekani zaua watu 5 Yemen

Posted on Aug 5 2012 - 10:15am by Mwemutsi Erick

Ndege ya kigaidi isiyo na rubani ya Marekani imetekeleza hujuma mashariki mwa Yemen na kupelekea zaidi ya watu watano kuuawa. Duru zinadokeza kuwa hujuma hiyo ilijiri Jumamosi katika mji wa Aden ambapo gari lililokuwa na abiria watano lililengwa. Kwa muda mrefu sasa Marekani imekuwa ikitumia ndege zisizo na rubani kushambulia raia huko Pakistan, Afghanistan, Yemen na Somalia kwa madai ya kukabiliana na magaidi. Hata hivyo raia wa kawaida ndio wahanga wakuu wa mashambulio hayo ya Marekani. Umoja wa Mataifa umelaani hujuma ya ndege hizo za kigaidi za Marekani na kusema ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.