Kenya; kiongozi wa MRC atiwa mbaroni

Habari kutoka mjini Kwale katika Pwani ya Kenya zinasema kuwa hali ya wasiwasi imetanda saa chache baada ya kutiwa mbaroni kiongozi wa kundi la MRC, Omar Mwamnuadzi.

Habari zaidi zinasema kuwa, wanachama wa MRC wamefanya shambulizi la kulipiza kisasi ambapo watu 2 akiwemo afisa wa serikali wameuawa.

Mkuu wa polisi katika mkoa wa Pwani, Aggrey Adoli amesema kuwa usalama umeimarishwa na kwamba msako mkali umeanzishwa ili kuwakamata wanachama wa kundi hilo linalopigania kujitenda eneo la Pwani. Ripoti zinasema kuwa, makabiliano makali kati ya polisi na walinzi wa Bw. Mwamnuadzi yalishuhudiwa mapema alfajiri ya leo nje ya nyuma ya kiongozi huyo wa MRC ambapo maafisa kadhaa wa polisi walijeruhiwa na walinzi wawili wa kiongozi huyo wakauawa kabla ya polisi kumkamata. MRC limesisitiza kuwa litavuruga shughuli za uchaguzi mkoani Pwani ingawa serikali imeapa kwamba itakabiliana na kundi hilo hadi mwisho

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

`
Design By : Tanzania Servers Technology