GODBLESS LEMA ASHINDA RUFAA YA KESI YAKE

Posted on Dec 21 2012 - 3:44pm by Mwemutsi Erick

Godbless Lema mara baada ya hukumu mahakamani leoAliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema leo ameshinda rufaa ya kesi yake. Mahakama imejiridhisha kuwa madai ya udhalilishaji hayakuathiri uchaguzi wala mlalamikaji (CCM). Tangu sasa Lema ni mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema. CCM wameamriwa kulipa gharama za kesi hii tangu ilipofunguliwa mpaka ilipoishia!

About the Author

Leave A Response