Fabio Capello awa kocha mpya wa Urussi

Chama cha mpira cha Urussi kimethibitisha habari za kua aliyewahi kua Kocha wa klabu ya Real Madrid na England Fabio Capello ndiye Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Punde baada ya kutangazwa Capello mwenye umri wa miaka 66 amesema shabaha yake ni ufanisi wa haraka. Ledngo langu ni kuiwezesha Urussi kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil, alisema Capello.

Nilipomaliza kazi ya England, nilikua na ghadhabu na nilitaka kuendelea kufanya kazi. Ukweli ni kwamba nataka kutimiza malengo yenu Urussi na kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Brazil.

Capello alikuwa kwenye orodha ndefu iliyokuwa na majina ya magwiji kama Harry Redknapp, ambaye chama cha mpira cha Urussi kilimtaka awe Kocha wake mpya.

Kocha huyo aliacha sifa ya kiwango kikubwa cha ushindi kuliko waliomtangulia England akishinda asili mia 67% ya mechi ingawa Timu yake ilipata shida kwenye mashindano ya Kombe le Dunia nchini Afrika ya kusini mwaka 2010 ilipoondolewa mapema na Ujerumani.

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

`
Design By : Tanzania Servers Technology