CHADEMA chaanza rasmi kuendesha Mabaraza ya Katiba nchini kote

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kuanzia jana kinaanza rasmi kuendesha Mabaraza ya Katiba, ambapo wananchi wote watashirikishwa kujadili na kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo;
 
1. Mikutano ya hadhara, itakayoanza leo katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiongozwa na     timu mbili za viongozi wakuu, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibroad Slaa. 
    
    Mikutano hiyo itafanyika nchi nzima. Ratiba ya mikutano yote, itatolewa kwa umma,     kupitia vyombo vya habari (mainstream & social media).
 
2. Kutuma ujumbe mfupi kwa simu. Mwananchi anaweza kutuma maoni yake ya Katiba     Mpya kupitia simu ya mkononi, kwenye NAMBA HII YA SIMU; 0789 24 82 24.
 
 
4. Mitandao ya kijamii, mf; Jamii Forums, facebooks, twitter, group emails, k.m mabadiliko, 
    wanabidii n.k, utaratibu wake utatolewa kwa umma, kupitia vyombo vya habari, ikiwa ni 
     pamoja na kuwekwa hapa, namna ambavyo Watanzania wote watashiriki kutoa maoni 
     yao kwa njia hii.
 
Tumaini Makene
CHADEMA Senior Information(Press) Officer
0752 691569/ 0688 595831

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

`
Design By : Tanzania Servers Technology