Aunt Ezekiel amefunga PINGU ya maisha

Hatimaye msanii  Aunt Ezekiel amefunga ndoa Oktoba 18, mwaka huu ambapo shughuli hiyo iliyofanyika Mwananyamala jijini Dar ilihudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki zake.
Aunt alifunga ndoa ya Kiislam na mchumba wake wa siku nyingi aitwaye Sunday Demonte anayefanya shughuli zake za kibiashara huko Dubai.

Paparazzi alizungumza na Aunt kabla ya tukio hilo ambapo alisema ni kweli amelazimika kutimiza zoezi hilo ili maisha mengine baada ya ndoa yaweze kuendelea.


“Ni kweli nimefunga ndoa leo ila Sunday hayupo, atawakilishwa na ndugu yake na sherehe kubwa itafanyika huko Dubai,” alisema Aunt.

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

`
Design By : Tanzania Servers Technology