ALICHOSEMA CHEGE KUHUSU USALAMA WAKE BAADA YA KUPATA AJALI USIKU.

Posted on Jul 18 2012 - 8:01am by Mwemutsi Erick

Msanii wa Kigoma All Stars Chege Chigunda usiku wa jana amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali kuhusu ajali hiyo zimesema kuwa usiku huo Chege alikuwa ametokea jijini Nairobi.

Akiongea na mtangazaji wa Clouds FM, Diva kwenye kipindi cha Ala za Roho, Chege amesema usiku huo wa saa nne akiwa kwenye gari alikutana pikipiki katika mtaa mmoja wa maeneo ya Temeke ambaye alimgonga na yeye kupata ajali hiyo.

Chege amepata majeraha kadhaa lakini anaendelea vizuri licha ya gari lake kuharibika vibaya maeneo ya mbele.

Haikuweza kufahamika mara moja hali ya mtu huyo aliyekuwa na pikipiki.

Kupitia mahojiano hayo mafupi Chege amewatoa hofu mashabiki wake kuwa hali yake ni nzuri na yupo salama.

Kupitia website yake,Diamond amempa pole mwanamuziki mwenzie wa Kigoma All Stars kwa Nampa pole sana msanii Chege Chigunda kwa Ajali mbaya ya gari,Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote yaliyotokea……

Tufuatilia kwa karibu taarifa mpya zinazohusiana na ajali hiyo.

Leave A Response